Leicester Yashinda Tuzo La Klabu Bora Ya Mwaka Uingereza

 Kocha wa Leicester pamoja na wachezaji wa timu hiyo na Mwogeleaji Michael Phelps baada ya kushinda tuzo za BBC
Klabu ya soka ya Leicester imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka kwa kuwashangaza wengi waliposhinda ligi ya Uingereza.

The Foxes kama inavyojiita ilishinda tuzo ya timu bora ya mwaka na mkufunzi wake Claudio Ranieri alitangazwa kuwa kocha bora baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda taji hilo.

Leicester ilianza kampeni ya kushinda taji hilo bila wengi kutarajia baada ya kushushwa katika ligi ya Uingereza mwaka 2014-15.

Walipoteza mechi tatu pekee katika msimu wa 2015-16 na wamefuzu kucheza kombe la vilabu bingwa Ulaya na kuendelea hadi raundi za muondoano.

 Kocha wa Leicester Claudio ranieri alishinda tuzo ya kocha bora wa mwaka Uingereza
  •  Kocha wa Leicester Claudio ranieri alishinda tuzo ya kocha bora wa mwaka Uingereza

Mwanzoni mwa mwezi Aprili, Leicester ilikuwa pointi saba juu katika jedwali la ligi ya Uingereza .

Mwaka mmoja kabla ,walikuwa chini ya jedwali hilo pointi saba pekee juu ya timu ambazo zilishushwa daraja.

Mwogeleaji wa Marekani Michael Phelps alishinda tuzo la mwanariadha bora wa olimpiki baada ya kushinda medali 23 za dhahabu.
Post a Comment
Powered by Blogger.