Lameck Ditto Ataja Faida Za Timu Za Wasanii Mitandaoni

 Ditto2
Msanii wa Bongo Fleva kutoka Morogoro Lameck Ditto anaefanya vizuri kwa sasa na wimbo wake wa Moyo Sukuma Damu amesema timu za wasanii zilizopo mitandaoni zinafaida kubwa sana kwa wasanii endapo zitatumika vizuri.


Image result for LAMECK DITTO

Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, amesema msanii kuwa na Timu ya mashabiki mtandaoni ni mtaji tosha kwani huenda msanii akauza kazi zake na kufanya Biashara nyingi tu kupitia mtandaoni.

Kuwa na timu mtandaoni ni jambo zuri sana kwani huenda ukafanya biashara zako nyingine mbali na kazi za kisanii pia ni rahisi sana kuwakutanisha mashabiki wako kwahiyo suala la kuwa na timu ni jambo zuri kwa upande wa kibiashara“Alisema Lameck Ditto.
Post a Comment
Powered by Blogger.