Lady JayDee amtambulisha mpenzi wake rasmi kupitia EATV Awards

 
Muimbaji huyo ambaye usiku jana aliambatana na mwanaume huyo kupokea tuzo ya Mwanamuziki bora wa kike, alilitumia jukwaa hilo kuwashukuru mashabiki wa muziki wake pamoja na kumtambulisha mwanaume huyo ambaye ni mgeni machoni pa wengi.

Baada ya shukrani kwa mashabiki na kutaka kuondaka alirudi jukwaani nakusema, “Nilitaka kusahau huyu ni baby wangu” kauli ambayo iliibua shangwe kubwa kwa mashabiki.Lady JayDee

Wiki chache zilizopita, muimbaji huyo kupitia Instagram alipost picha ya mwanaume huyo na kuandika:

“Big shout out kwa Coastal air Kwa kufanikisha safari yangu kwenda honeymoon #ZanzibarIsland,”

kauli ambayo ilitafsiriwa huwenda wawili hao wamefunga ndoa.

Jay Dee hakuwahi kuweka wazi mahusiano yake tangu aachane na aliyekuwa mue wake, Gardiner G Habash.
Post a Comment
Powered by Blogger.