Lady Jay Dee adai Sio lazima kuwa na record label kwa sababu msanii fulani anayo

 Buff Bantam Hen {Gallus gallus domesticus} with nine of her ten chicks, 2-days-old. The tenth chick is under her


Msanii mkongwe wa muziki Lady Jay Dee amesema hana mpango wa kuanzisha record label kwa kuwa kuna baadhi ya wasanii wanafanya hivyo.

Alisema hayo wiki hii wakati alipo watembelea wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Kampasi ya Mlimani) na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu muziki.

Muimbaji huyo alisema wasanii wengi wanaanzisha record label kwa kuwa wamewaona wasanii fulani wamefanya hivyo.

“Sio lazima kila mtu awe na record label,” alisema Lady Jay Dee. “Kila msanii ana namna ambavyo anafanya kazi. Kwahiyo suala la record label kwa sababu msanii fulani anayo sio lazima,”

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka wasanii wachanga kuonyesha vipaji vyao kwanza kabla hawajakimbilia kuoamba msaada.

Pia alisema yeye kabla ya kuanza kupata nafasi ya kuonyesha kipaji chake alianza kupiga simu redioni na kuimba live ili kuonyesha ni kitu alichonacho.
Post a Comment
Powered by Blogger.