Kocha Jose Mourinho akana kukwepa kodi..
Akiwa anakabiliwa na changamoto za kutopata ushindi katika mchezo wa soka, sasa kocha wa Manchester United, Jose Mourhino, atawajibika kujibu tuhuma za ukwepaji wa kodi.

Taarifa hiyo imekuja baada ya kuchapichwa kwenye mtandao wa `football leaks`, akiwa mmoja wa watu wanaolipwa vizuri katika mchezo wa soka pamoja na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, wanaotuhumiwa kuficha fedha zao nje ya nchi wazoishi ili kukwepa kodi.

Huenda kocha huyo akajibu mashtaka kwa kuficha kiasi cha pauni milioni 10 katika Visiwa vya British Virgin Islands.

Katika taarifa yake iliyokuwa katika maandishi baada ya mchezo dhidi ya Everton, Mourinho amekanusha tuhuma hizo.

Mourinho amelipwa jumla ya pauni milioni 90 akiwa na klabu za Porto, Chelsea, Inter Milan, Real Madrid na sasa Manchester United.

Inaaminika amelipa kodi kila wakati kutokana na mapato yake, lakini anatuhumiwa kutorosha mamilioni aliyolipwa kutoka kampuni mbalimbali yanayotokana na brand yake.

Aliwahi kukiri kukwepa kodi akiwa Chelsea na baadaye kulipa pauni 288,300.

Katika taarifa hiyo ya kiuchunguzi inaonyesha kuwa, akiwa Inter Milan, alikotwaa taji la Mabingwa wa Ulaya alilipwa kiasi cha pauni milioni 15.2 kwa mwaka.

Alipohamia Real Madrid, kiasi kidogo alicholipwa kwa mwaka ni pauni milioni 12.8, ikiwa ni pamoja na kutumia brand yake na bonasi.

Mourhino amesema tayari amewasilisha nyaraka zake nchini Italia, Hispania na England kwa wanaohusika na kwamba hana lolote la kuficha.
Post a Comment
Powered by Blogger.