Klabu Ya Arsenal yaondolewa kwenye mashindano ya Kombe la EFL.


Magoli ya Jordy Clasie na Ryan Bertrand yameitupa nje Arsenal kwenye kombe la EFL na kuipeleka Southampton hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1987.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ambaye hajawahi kutwaa taji hilo katika miaka yake 20 aliyoishi London, alifanya mabadiliko ya wachezaji 10 kwenye kikosi cha Arsenal kilichoshinda 3-1 dhidi ya Bournemouth kwenye mchezo wa Premier League Jumapili iliyopita.

Southampton ambao wameshinda mara moja katika michezo 23 waliyosafiri kuifata Arsena, walistahili ushindi na watacheza dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza itakayochezwa kwenye uwanja wa St Mary January 9 mwaka ujao.
Post a Comment
Powered by Blogger.