Kiungo wa Man United Paul Pogba amechukizwa na uzushi dhidi yake.Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Paul Pogba amekerwa sana kwa taarifa ambazo yeye anadai kuwa ni za upotoshaji ambazo zinaelezea juu ya tabia yake kipindi akiwa na Juventus kabla ya kwenda United.
Kiungo huyo ambaye aliutumia muda wake wa miaka minne akikipiga pale Turin. Na kuiwezesha Juve kubeba mataji ya Ligi ya Serie A kwenye kila msimu kabla ya yaku kurudi tena Old Trafford kwa ada ambayo ilivunja rekodi ya usajili.

Ilikuwa inasemekana kwamba wakati akiondoka alidai kuwa ni kama anakwenda mapumzikoni na baadaye atarudi. Hata hivyo, kwa upande wake anadai kwamba yeye hajawahi kuongea kitu kama hicho.

Pogba anasema yeye alirudi Manchester United kwa sababu ni klabu ambayo amekulia na alikuwa anajisikia anarudi nyumbani kwake.
Post a Comment
Powered by Blogger.