Kiungo wa Man City Yaya Toure adai hakulewa maksudi.


Kiungo wa Manchester City na Ivory Coast, Yaya Toure ameendelea kudai kuwa hanywi pombe licha ya kukubali kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.
Toure alifunguliwa mashtaka ya kuendesha gari akiwa amevuka kiwango cha ulevi wiki mbili zilizopita. Mbele ya mahakama, kiungo huyo aliamua kutopinga shtaka hilo ingawaje amedai hakunywa pombe kwa makusudi. hajapinga shtaka la kuendesha gari akiwa amelewa wiki mbili zilizopita ingawaje amesema hakunywa kwa makusudi.
“Siku zote nimekuwa nikikataa pombe ya aina yoyote, anayenifahamu na anayenifuatilia katika soka bila shaka atakuwa ameniona nikikataa shampeni ya Mchezaji Bora wa Mechi kwa sababu ya kuheshimu imani yangu.”
” Suala hili limemalizika mahakamani Jumatatu. Kwa kuwa nilivuka kiwango kilichoruhusiwa wakati nilipopimwa, niliamua kutopinga shtaka.
“Ni muhimu kwangu kwamba niliiambia mahakama sikulewa kwa  makusudi. Katika hukumu yake, hakimu alikubali kuwa sikulewa kwa makusudi. ”
” Kuendesha gari ukiwa mlevi ni kosa kubwa na ingawa sikulewa kwa makusudi, nakubali kosa pamoja na faini na pia naomba radhi. “
Post a Comment
Powered by Blogger.