Tetesi Za Kanye West Na Kim Kutengana Zina Ukweli Wowote?, Soma Hapa Stori Kamili.Taarifa sio nzuri kutoka kwenye ndoa ya mastaa Kanye West na Kim Kardashian, Fununu za wawili hao kutalakiana ndio stori iliyopo kwenye headlines za mitandao mbalimbali.

 Mtandao wa E! umefanikiwa kuzinyaka za ndani sana kutoka kwa mtu wa karibu na familia hiyo na amekanusha taarifa hizo.


“Nilikua nikiongea na Kim na Kanye muda mfupi uliopita, hakuna hata mmoja kati yao ambaye anaonekana kuwa na tatizo na mwenzake, kifupi sijasikia chochote kuhusu ishu ya talaka.”  Sosi huyo aliuambia mtandao huo.


“Kim bado anasawazisha akili yake tangu lile tukio la kuvamiwa mjini Paris huku Kanye akiendelea kuimarisha afya yake baada ya kuumwa ghafla siku chache zilizopita, stori ya wawili hao kutengana ni ya uongo na inapaswa kupuuzwa” aliongeza sosi huyo.


Nedy Music Azungumzia Kolabo Yake Na Christian Bella 
Post a Comment
Powered by Blogger.