Kasper Schmeichel: Kipa wa Leicester arejelea mazoezi

 Kasper Schmeichel
Golikipa wa Leicester Kasper Schmeichel amerejelea mazoezi katika klabu yake baada ya kuumia mkono mwezi Novemba.

Kuna uwezekano huenda akaweza kucheza mechi ya Jumamosi ugenini Stoke City.

Kasper Schmeichel 
Kasper Schmeichel alicheza katika mechi zote 38 za Leicester City ligini msimu uliopita na kuwasaidia kushinda taji la ligi 

Schmeichel, 30, aliumia mkono wa kulia wakati wa mechi yao Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya FC Copenhagen tarehe 2 Novemba ambayo ilimalizika kwa sare tasa. Hata hivyo alicheza mechi hiyo hadi mwisho.

Leicester wameshinda mechi mbili pekee kati ya nane walizocheza ligini na katika michuano ya kombe la ligi tangu wakati huo.

"Kasper alishiriki mazoezi vyema leo," kocha wa Leicester Claudio Ranieri alisema Alhamisi.

Schmeichel alichezea Leicester mechi 38 za ligi msimu uliopita na kumaliza mechi 15 kati ya hizo bila kufungwa.
Post a Comment
Powered by Blogger.