Jeshi la Polisi Kutoa Msimamo wake Kuhusu Kauli za Mzee wa Upako Kwamba Waliomchafua Watakufa Mwakani


Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi 2017, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo. 

Kauli hiyo ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na kumfanyia fujo jirani. 

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro jana  alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa sikukuu na atatolea ufafanuzi leo. 

“Anasema hao waandishi watakufa kabla ya Machi 2017 kwani yeye Mungu? Hilo ni suala zito, tumeandaa mkutano na waandishi wa habari tutalizungumzia suala hilo kesho (leo),” alisema Kamanda Sirro.

 Katika kauli hiyo, Mzee wa Upako alisema kila mwandishi aliyemuandika vibaya ikifika Machi mwakani hatakuwa hai na kama wataendelea kuishi, ataacha kazi ya kuhubiri injili na kwenda kuuza gongo.
Post a Comment
Powered by Blogger.