Je Unahitaji Kolabo Na Ben Pol Mwakani? Basi Jipange Na Mkwanja Huu

 
Ben Pol ni moja ya wasanii waliofanya vizuri sana kwa mwaka 2016 kwenye tasnia ya muziki hapa Bongo, mbali ya wimbo wake wa Moyo Mashine Ben Pol amefunga mwaka vizuri kwa Kushirikishwa na Darassa kwenye wimbo wa Muziki, wimbo ambao nadiliki kusema ni wimbo wa Taifa.

Lakini je? kwa wasanii wenye lengo la kufanya nae kolabo kwa mwakani watampataje?

Image result for ben pol

Kwa msanii anaehitaji kolabo na Ben Pol ni rahisi tu cha kufanya ni kujiandaa kwa mkwanja wa kiasi cha Dola 5000 tu yaani kama Milioni 10 hivi.

So hapo utakua umefanikiwa kufanya nae kolabo, kwani leo Kupitia ukurasa wake wa Twitter Ben Pol ameweka wazi kwa wasanii watakaohitaji kufanya nae kolabo kwa kuandika

Kuelekea 2017 bei yangu ya Collabo itakuwa $ 5000. So kama una project na mimi tuwasiliane before 31st Dec 2016. Thanks

Post a Comment
Powered by Blogger.