Jay Dee afunguka kuhusu kustaafu muziki


Mkongwe wa muziki nchini mwanadada Lady Jay Dee, amewajibu wanaotaka astaafu muziki, na kusema kuwa ataendelea kuwepo kwenye game ya bongo fleva na kwamba hana mpango wa kuacha muziki.

 

Jay Dee ametumia nafasi aliyopata katika tuzo za EATV kutoa jibu hilo, huku akisema ataendelea kuwaburudisha mashabiki zake na muziki mzuri, na kamwe hatachoka.

Akizungumzia Tuzo aliyoipata ya Mwanamuziki bora wa kike, Jay amesema ni hatua nzuri kwake kuendelea kumng'arisha huku akitoa pongezi kwa EATV kwa maandalizi mazuri ya tuzo hizo.

Msikilize hapa akifunguka....

Post a Comment
Powered by Blogger.