Izzo Bizness Adai Hahofii Kuachia Ngoma Kipindi Wasanii Wengi Wameachia Zao

 
Kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka 2016, tumeshuhudia Wasanii wa Bongo wakitoa ngoma kali ambazo zimekuwa zikipendwa sana mtaani na zinachezwa sana kwenye radio na TV Stations za hapa Bongo.

Hali hii imewafanya baadhi ya wasanii kusita kutoa kazi zao mpya kwa kuogopa kufichwa na kazi za wasanii wenzao ambazo zinafanya poa kwa sasa. Lakini suala hilo halifikiriwi na Izzo Bizness Nna kundi la The Amazing.

Izzo Bizness ambae yeye na member mwenzake wametoa kazi yao mpya ya Umeniweza, amedai hawawezi kusita kutoa Ngoma kisa kuna ngoma kali za wasanii wengine zinafanya vizuri.

“Msanii bora unajipima kwa wasanii wenzako, huwezi ukawa unasubiri hamna kitu ndio utoe ili wewe unonekane kwamba una nyimbo nzuri. Unatoa nyimbo kwenye sehemu nzuri,watu wanajua mziki mzuri,” alisikika Bizness ndani ya Dizzim Online.

Izzo ambaye tarehe 25 anasheherekea siku yake ya kuzaliwa ambayo pia ni siku ya Christmas,amepanga kwenda kwao Mbeya Kufanya tamasha la kila mwaka la Home Sweet Home, ambapo kupitia tamasha hilo,huibua pia vipaji vya wasanii wachanga wa Mbeya na kuwapa nafasi ya kurekodi Dar es Salaam.
Post a Comment
Powered by Blogger.