Izzo Bizness & Abela Music (The Amazing) Wajipanga Kwenda Kimataifa

 


Mwaka 2016 tumeshuhudia wasanii wengi wa Bongo Flava wakiweka nguvu na akili zaidi kwenye kazi zao ili kuliteka soko la kimataifa.

Kundi la The Amazing linaloundwa na wasanii Izzo Bizness na Abela Music ni kundi lililotambulishwa kwenye game miezi 6 iliyopita na sasa wana lengo la kwenda kimataifa zaidi kupitia kazi yao mpya waliyoiachia wiki hii iitwayo Umeniweza.

 
The  Amazing

Member wa kundi hilo, Izzo Bizness akipiga story na  Dizzim Online amesema kuwa kwenye kazi yao hiyo mpya wameonyesha viwango vyote vya kimataifa na wanasubiri kuituma kazi hiyo kwenye media za nje waone kama itapokelewa.

"Unajua muziki ni Universal language, kwahiyo viwango vyote vya kwenda soko la kimataifa tayari vimeonyeshwa humo kwenye ngoma. kwahiyo issue ni kupush na kujaribu kuwatumia kusubiri jamaa wanasemaje", amesema Izzo Bizness.

Kwa sasa kundi la The Amazing limekuwa moja ya makundi yanayo tazamwa zaidi kwenye muziki hapa Tanzania.
Post a Comment
Powered by Blogger.