Idris Sultan ajibu hivi juu ya swali kuhusu Diamond Platnumz na AliKiba

 
Mchekeshaji Idris Sultan alikutana na swali linalowapa ugumu watu wengi wakiulizwa. Moja ya swali hilo hili hapa.

SeetheAfrica inakusogezea swali hili kama lilivyoulizwa na mtangazaji wa kituo cha redio moja nchini uganda usiku wa Dec 9  kwenye ugawaji wa tuzo za ASFA201.


Swali hilo lilisikika hivi.. Kwa upande wako Nani mkali kati ya Kiba na Diamond?, kutokana na uzito wa swali hilo Idris aliamua kujibu kama ifuatavyo. Wote ni marafiki zangu, lakini sawa, nafikiri wote wanatofautiana, nitajibu kwa kuwatofautisha, sio kama ulivyoniuliza.Yupi anaimba vizuri? Nitasema Ali Kiba. Yupi ana ‘hustle’ sana? Nitasema Diamond. Yupi anapiga hela nyingi? Bila shaka ni Diamond. Yupi ni mpole, na ana uwezekano wa kuingia peponi? Nitasema Ali Kiba. Alimaliza Idris Sultan alipofanya mazungumzo na mwandishi mmoja nchini Uganda.
Post a Comment
Powered by Blogger.