Huu Hapa Ujumbe Wa Madee Kwa Wanao Mpost Chid Benz Mtandaoni


Kumekuwa na tabia ya ajabu inayo endelea mitandaoni especially kwenye mtandao wa instagram, kwa kupost picha au clip zinazo muonesha Rapa Chid Benz.Wengi wamekuwa wakilalamika kwa kutoa maoni yao na mitazamo yao kwa kitendo hicho kwenye mtandao huo huo kuhusu jambo hilo.

Leo December 27, Msanii Madee kutoka Tip Top Conection kupitia ukurasa wake wa Twitter katoa ujumbe unaoonesha wazi kuchukizwa na kitendo cha kupost picha au video za Rapa Chid Benz akiwa katika hali aliyonayo kwa sasa.

Ujumbe huo ulisomeka hivi "Hawa wanaompigapiga picha ChidiBenz na kupost kwenye mitandao yao lengo lao kubwa ni nini? mbona tunazidi kumdhalilisha? au mnataka kiki?

Jambo hili limewafanya mashabiki kuanza kutengeneza maswali mengi kwa Madee kwamba kwa kusema “Madee anatatizo na Solo Thang au”?, Maswali hayo ambayo wanajiuliza mashabiki yamekuja baada ya kuunganisha tukio la Rapper Solo Thang hivi karibuni kwa kupost kipande cha video katika kurasa yake ya Instagram akiwa na Chid Benz huku akiandika ujumbe wa kusikitishwa na hali aliyokuwanayo Chidi.

“Met with my Young brother Chid Benz last night almost cried, I dont judge, no matter what still my hommie, tumeongea sana, tuzidi kumuombea Mola”Post a Comment
Powered by Blogger.