Hii Hapa Orodha Ya Mastaa 5 Walioishia Kuvishana Pete Bila Ndoa 2016

 Image result for Miley Cyrus & Liam Hemsworth
Tupo mwishoni mwa mwaka, kama kawaida nakuletea tukio muhimu lilopata kutingisha kwa mwaka huu.

Hii hapa listi ya mastaa wa mbele ambao walivalishana pete kwa lengo la kuoana, lakini ndoto zao hizo hazikukamilika hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Orodha hii hapa

Mariah Carey na James Packer


Image result for Mariah Carey & James Packer

Taarifa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii duniani zilienea habari za nyota wa muziki nchini Marekani, Mariah Carey kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, bilionea James Packer raia wa nchini Australia.

Uhusiano wa wawili hao ulianza tangu 2015 mara baada ya Mariah kuachana na baba watoto wake Nick Cannon, ambaye alifanikiwa kupata naye watoto wawili mapacha, hivyo kuachana kwao kulimpa nafasi mfanyabiashara huyo kutoka nchini Australia kuonesha jeuri ya fedha.

Hawakuchelewa kuonesha uhusiano wao, hivyo James aliamua kununua pete ya dhahabu yenye thamani ya zaidi ya bilioni 21 za Kitanzania, hapo hapo kutangaza ndoa ambayo waliweka wazi kuwa kabla ya mwaka 2016 kumalizika watakuwa wamefunga.

Wengi walikuwa wanaisubiri ndoa hiyo kwa hamu kutokana na fedha zilizotumika kwenye kununua pete, lakini mambo yalikuwa tofauti siku chache baadaye, ambapo ndoto za wawili hao za kufunga ndoa mwaka huu zikafikia mwisho mwezi Oktoba. Kwa sasa wamebaki kuwa na mgogoro wa kupotezana muda.

Blac Chyna na Rob Kardashian

 Image result for Blac Chyna & Rob Kardashian

Blac Chyna ni mwanamitindo maarufu nchini Marekani ambaye alifanikiwa kupata mtoto wa kwanza akiwa na uhusiano na rapa Tyga, lakini Januari mwaka huu aliweka wazi kuwa anatoka na kaka wa Kim Kardashian, Rob Kardashian.

Aprili mwaka huu, mrembo huyo alivishwa pete na mchumba huyo huku wakitangaza kutaka kufunga ndoa Desemba mwaka huu mara baada ya kufanikiwa kupata mtoto wao, kwanza walianza kwa kufanikiwa kupata mtoto mapema Novemba na ndipo watu wakawa wanasubiri ndoa ya wawili hao Desemba.

Kwa sasa imebaki stori kwa kuwa wawili hao tayari wameachana mapema Desemba hii kwa madai kwamba familia ya Rob amekuwa na michepuko mingi, hataki ushauri kutoka kwa mrembo, pamoja na migogoro ambayo inaendelea ndani ya familia hiyo ya Kardashian, kwa sasa kila mmoja anaishi kivyake japokuwa wakiwa na mtoto wa mwezi mmoja.

Nicki Minaj na Meek Mill

 Image result for Nicki Minaj & Meek Mill

Wawili hao wanafanya muziki wa Hip Hop nchini Marekani, walianza uhusiano wao tangu 2015, lakini mapema mwaka huu walitangaza kutaka kufunga ndoa mara baada ya Meek Mill kumvisha pete mchumba huyo.

Mapema Novemba mwaka huu kulikuwa na taarifa kwamba wawili hao wameachana, lakini hakuna ukweli huo, bado wapo pamoja na wanaendelea na ratiba yao ya kutaka kufunga ndoa.

Ukweli ni kwamba dalili za ndoa hiyo kufanyika mwaka huu hazipo japokuwa wapo kwenye uhusiano, hivyo kwa wiki hii moja iliyobaki kuingia 2017 ni asilimia chache wawili hao kufunga ndoa.

Miley Cyrus na Liam Hemsworth

 Image result for Miley Cyrus & Liam Hemsworth

Wawili hao ni wapenzi wa muda mrefu tangu 2012, na wamekuwa wakiachana na kurudiana ambapo ni zaidi ya mara mbili sasa, lakini Januari mwaka huu waliweka wazi kuwa wanataka kufunga ndoa lakini cha kushangaza hadi sasa dalili za kufunga ndoa hazipo kabisa wamebaki kuvishana pete.

Jason Statham na Rosie Whiteley

Image result for Jason Statham & Rosie Whiteley

Hao ni nyota wa filamu, wamekuwa kwenye uhusiano wa wazi tangu 2010, lakini mapema mwaka huu Statham alifanikiwa kumvisha pete ya uchumba mrembo huyo ambapo hafla hiyo ilifanyika nchini Thailand, lakini hadi sasa kimya hakuna dalili zozote za ndoa yao.
Post a Comment
Powered by Blogger.