Hawa ndio watakaosimamia Mali za Donald Trump akianza kutekeleza majukumu ya Uraisi.

Trump

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema biashara zake zitasimamiwa na kuendeshwa na wanawe wawili atakapokuwa rais.

Wanawe hao ni Donald Junior na Eric, ambao tayari wamekuwa wakitekeleza majukumu muhimu katika uendeshaji wa baadhi ya biashara.

Trump amesema atawakabidhi biashara hizo kabla ya kuapishwa kwake na kwamba hakuna mikataba mipya ya kibiashara ambayo itaingiwa na kampuni zake kipindi ambacho atakuwa anahudumu kama rais.Eric TrumpWakosoaji wa rais huyo mteule wanasema bado atakuwa hatarini ya kutokea kwa mgongano wa maslahi iwapo hataachilia umiliki wa biashara zake.

Post a Comment
Powered by Blogger.