Hatimae John Legend amchana bosi wake Kanye West, kisa hiki

 
 Kitendo cha Kanye West kukutana na Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, kimewakera watu wengi, wakiwemo watu wake wa karibu.

Mmoja wao ni John Legend, ambaye amedai kuwa hatua hiyo ya bosi wake wa GOOD Music, imempa kiki Trump.

Legend ametoa msimamo wake kwenye kipindi cha Clique kinachoruka kwenye kituo kimoja cha runinga cha Ufaransa Jumanne hii. Alipoulizwa kama yupo tayari kufanya mazungumzo na Trump, jibu lake lilithibitisha kuwa ni ndoto.

“I don’t think it’s impossible to talk to him about issues, but I won’t be used as a publicity stunt. I think Kanye was a publicity stunt,” alisema Legend.

Aliongeza, “I’m pretty disappointed with Kanye that he says he would have voted for Trump. I think Trump has been corrosive, his message has been corrosive to the country.”
Post a Comment
Powered by Blogger.