Hatimae AT ajikojolea kisa tuzo za Alikiba Eatv AwardsMsanii wa miondoko ya mduara AT jana kabla ya kutolewa kwa tuzo za #EATVAwards aliweka nadhiri kuwa endapo msanii Alikiba akishinda kwenye tuzo hizo kwa furaha basi yeye atakojoa kitandani na kuposti picha ya tukio hilo.

Baada ya kuweka nadhiri hiyo usiku wa jana Alikiba aliibuka na ushindi kwa kubeba tuzo tatu na kufanya kuwa msanii wa kwanza katika tuzo hizo kuchukua tuzo nyingi kwa wakati mmoja, hivyo baada ya ushindi huo AT alikamilisha ahadi yake ya kukojoa kitandani na kuweka picha kama uthibitisho wa furaha aliyonayo baada ya mkali Alikiba kuibuka na tuzo tatu.

Mbali na hili AT amesema kwa sasa yeye yupo likizo katika muziki hivyo hawezi kutoa kazi yoyote mpaka mwakani na kusema yeye na Alikiba ni kati ya wasanii wakali wenye uwezo wa kutunga nyimbo kali na kukaa muda mrefu pasipokuwa na nyimbo na wakafanya poa pindi wanaporudi."Bado nipo likizo hadi 2017 kama msanii wako mkali aimbe nyimbo kama 'Nipigie au Makimuga' hadi leo zipo na uhai hadi miaka 50 ijayo. wakati mwingine mashabiki muwe wazima wa akili timamu kufuatafuata mkumbo kwenu siku moja kutawatia kiharusi kuna wasanii hawawezi kukaa hata mwezi kimya ulizeni kwanini? Anaejiamini haogopi wingi wa wasanii anaogopa kufanya kitu chini ya uwezo wake". Aliandika AT
Post a Comment
Powered by Blogger.