Fid Q Adai Kumkataa Man Fongo Ni Kosa Kubwa

 13774606_1667293583597820_215343024_n
Rapa Fid Q ambaye anafanya vyema na wimbo wake 'Sumu' pamoja na 'Roho' amefunguka na kusema kuwakataa wasanii wa singeli kama Sholo Mwamba na Man Fongo na 'Impact' walizonazo kwenye jamii ni sawa na kuikosea kabisa tasnia nzima ya muziki wa bongo.

Fid Q anadai kuwa Man Fongo ni mapinduzi ya muziki wa kizazi kipya.

Fid q

"Unapoongelea Man Fongo unaongelea mapinduzi ya muziki mpya wa kizazi cha sasa cha bongo, unajua kuna bongo fleva muziki wa kizazi kipya lakini kuna singeli muziki wa kizazi kipya cha kizazi kipya hiki. Kwa hiyo Man Fongo ndiye mfalme wao lakini nisimsahau kuna Sholo Mwamba pia, hivyo kuwakataa wasanii hawa na impact waliyonayo ni kukosea kabisa 'Indusrty' nzima kiujumla yaani ni sawa na kusema ndege haziendi angani zinapita kwenye reli". Alisema Fid Q
Post a Comment
Powered by Blogger.