Ferooz Aja Ana Kundi Lake Jipya, Lifahamu Hapa


Baada ya kimya cha muda mrefu na kurudi miezi kadhaa nyuma na ngoma ya "Nimejifunza" kwenye ramani ya Bongo Fleva lakini bila ya kutusua kiivyo, sasa Ferooz anakuja kivingine.

Ferooz ameamua kuja na kundi jipya ambalo huenda likaanzia pale ambapo Daz Nundaz iliishia. Kundi hilo liitwalo Wabeshi lipo katika studio za Bongo Records kurekodi ngoma zake.

 

Majani ambaye miezi ya hivi karibuni amekuwa busy studio kurekodi miradi mipya, ameweka picha ya wakali hao Instagram na kuandika: Ferooz’s new group just finished recording vocals. ( The new Daz Nundaz )and all of them are artist!! #Wabeshi.

 

Majani anafahamika kwa kuwa na mchango mkubwa kwa kundi la Daz Nundaz ambalo lilitoa wasanii wakubwa akiwemo Ferooz na Daz Baba.
Post a Comment
Powered by Blogger.