Elizabeth Michael ‘Lulu’ atwaa tuzo hii Swahili fashion

 Maonyesho ya mitindo ya mavazi ya Swahili Fashion Week 2016 yalianza jijini Dar es salaam, ambapo wabunifu kutoka sehemu mbali mbali Afrika wamepata fursa ya kuonyesha ubunifu wao.

15037227_10153938213765986_7960407558636878994_n

Maonyesho hayo ambayo yalianza siku ya tar 2 Desemba nakuendelea mpaka tarehe 4 Desemba 2016, yamekuwa na mafanikio makubwa kutoa fursa kwa wabunifu kutoka nje ya mipaka ya nchi yao na kukutana pamoja kuonyesha vipaji vyao vya ubunifu.

Good news ni kwamba, Kwenye tukio hilo lililofanyika usiku wa tar 4 Desemba 2016, muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) alijinyakulia tuzo ya mtu maarufu kwenye mitindo (Most stylish icon).


14550112_686784161492640_5179799325697376256_n 


Sambamba na hayo tukio lililoibua hisia kubwa ni pale tuzo ya ‘Life achievement’, ambayo ilikwenda kwa mwandishi na mpiga picha maarufu hapa nchini, Muhidi Issa Michuzi.
Post a Comment
Powered by Blogger.