Denzel Washngton Afunguka Haya Kuhusu Tuzo Za Oscar

Related image
Mwigizaji maarufu kutoka Nchini Marekani Denzel Washington amefunguka mengi kuhusu tuzo za filamu za Academy Awards Maarufu kama Tuzo za Oscar kwa mara ya kwanza tangia Will Smith azipe kisogo Tuzo hizo kwa miaka miwili mfululizo.


Densel Washngton alinukuliwa na Jarida la The Hollywood Reporter akisema Tuzo za Oscar zina upendeleo sana kwani hata vipengele vyake vimewekwa kwa kujuana juana lakini pia amesisitiza kuwa yeye haamini kwenye ubaguzi wa rangi bali anaamini kwenye kujuana zaidi hususani kwa waandaji wa tuzo hizo.
Mshindi huyo wa tuzo ya mwigizaji bora mwaka 2002 na mwigizaji bora msaidizi katika filamu ya 2990 mbali ya kuchaguliwa kwenye Vipengele Vinne mwaka huu bado anaona kuna mapungufu makubwa kwenye tuzo hizo maarufu zaidi Duniani.

Tuzo za Oscar zimeingia kwenye kashifa nzito za kibaguzi kwa miaka mitatu mfululizo baada ya kuonekana kuwa na upendeleo kwenye uteuzi wa waigizaji hususani kwenye Vipengele kumeonekana Waigizaji weupe wakipata shavu zaidi kuliko wale wenye asili ya Kiafrika.

Tuzo za Oscar zitatolewa mwakani Februari 29
Post a Comment
Powered by Blogger.