Darassa, Bill Nas kuwasha moto EATV AWARDS 2016 , Viingilio hivi hapaShangwe za usiku wa EATV AWARDS zinazidi kutawala mjini ambapo leo wanasanii watakaowasha moto jukwaa hilo kwa kutoa burudani kali wametajwa.

Burudani hizo zitapambwa na msanii ambaye hivi sasa ndiye 'talk of the town', ambaye pia wimbo wake nusura utoe roho za watu kwa ajali baada ya dereva kuacha usukani na kucheza wimbo wa 'MUZIKI' wa Darassa au 255 Champion.

Darassa atatoa burudani za kufa mtu za kufungia mwaka, sambamba na mzee wa kuzima simu feki na kupiga CHAFU POZI, Bill Nas.

Kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki kwa pamoja itashuhudia wasanii hao wakitoa burudani, pamoja na wasanii wengine ambao watatangazwa siku zijazo, huku watu mbalimbali maarufu wakihudhuria sherehe hizo, ambao wengine itakuwa ni 'suprise'.

Kwa tiketi za VIP zitapatikana kwa shilingi elfu 50, huku zile za kawaida zitapatikana kwa shilingi elfu 20, na iwapo mtu atanunua kwa M-PESA, tiketi za VIP atanunua kwa shilingi 45, 000 na kawaida akinunua kwa shilingi 18,000.

Tiketi hizo zitapatikana, Samaki Samaki City Centre, Masaki na Mlimani City, Namanga Best bite na studio za East Africa TV na Radio.

Sherehe hizo zitahudhuriwa na watu mbalimbali maarufu kutoka ndani na nje ya nchi, huku wengine wakiwa ni 'suprise' kwa wadau na mashabiki watakaofika, huku jukwaa likisimamiwa na mkali wa MIC kabla hajazaliwa , Salama Jabir.
Post a Comment
Powered by Blogger.