Darassa atoa ushauri huu kwa Mashabiki wake


 Wiki hii imeanza kwa Matukio mbalimbali lakini tukio kubwa ambalo limeshangaza umma ni lile la Dereva aliyetambulika kwa jina la Juma Said Mkazi wa Dodoma aliyekuwa akicheza Muziki huku akiachia usukani.


Wimbo aliokuwa akicheza ni wimbo wa Darassa wimbo wake mpya wa Muziki,wimbo ambao umekuwa gumzo kila kona ya mtaa yaani kwenye Radio ndiyo wimbo unaoombwa kwa sasa kuliko wimbo wowote ule Tanzania.

Image result for darassa

DARASSA

Leo kupitia kipindi cha Planet Bongo Cha EA Radio Darassa amesema anashindwa kutambua wale mashabiki muhemko wa kupenda kitu mpaka kuhatarisha maisha kwani walichofanya ni kinyume na Sheria.

“Nikinyume na sheria kwa mtu yeyote yule na ni hatari hata kwa maisha yao ni vijana wanaojituma nimewafuatilia nimeongea na rafiki yao wa karibu jana walikuwa kituo cha polisi Manyoni jana walitolewa wakaenda Itigi ni watu wanaofanya mishe zao nadhani tatizo la feelings tu so nawashauri mashabiki wapunguze hiyo kitu ili kuepusha matatizo kama haya” Alisema Darassa.

Tazama Tukio la Dereva huyo akiendesha Gari huku akifurahia hit song ya wimbo wa Muziki wa Darassa.


Post a Comment
Powered by Blogger.