Country Boy Awataka vvjana Wajifunze Hili Kutoka Kwa Young Dee


June mwaka huu, rapper Young Dee alikiri mbele ya waandishi wa habari kuwa alikuwa akitumia madawa ya kulevya na akatangaza uamuzi wa kuachana na matumizi ya dawa hizo ili aweze kurudi vyema katika muziki.

Ulikuwa ni uamuzi wa busara na wa kishujaa sana,kwani vijana wengi wamekuwa wazito kufanya maamuzi kama hayo pindi waingiapo kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na tunaona wengi wao wakitaabika hadaharani. Ushujaa alioufanya Young Dee,umemfanya Rapper Country Boy kuamini kuwa vijana wengi wanapaswa kujifunza kutoka kwake.

Akipiga story na Dizzim Online, Country Boy amesema kuwa kipindi alichokipitia Young Dee ni Kipindi cha kujifunza zaidi kwa vijana wa kisasa. “Mimi naona ilikuwa ni kipindi cha kujifunza kwake kimaisha na sisi kama vijana kuona kwa sababu kila kitu kiliweza kuonekana..unaweza ukaanza kwa furaha, mwisho wa siku ikaja kukutesa", amesema Country Boy.

 Pia Country Boy amedai kitendo cha Young Dee kuficha kumwambia kipindi alichokuwa anatumia madawa,ni kitu ambacho anakiheshimu sana na kinafanya azidi kumheshimu
Post a Comment
Powered by Blogger.