Country Boy Adai Mtu Chee Inarudi Upya


Moja kati ya makundi ya waasanii wa hip hop yaliyowahi kufanya vizuri, kipindi cha nyuma, ni Mtu Chee. Kundi hilo liliundwa na Country Boy na Young Dee na Stamina.

Ni muda sasa tangu wafanye kazi ya pamoja kama kundi. Hii ilitokana na kutofautiana wao kwa wao.

 Image result for mtu chee

Hata hivyo sasa Country Boy ameiambia Dizzim Online kuwa kundi hilo liko mbioni kurudi.
“Tunajaribu kurudi na kutengeneza urafiki upya na ukaribu kati yetu then tutafanya kazi,” amesema.

Amesema ili kundi hilo liweze kurudi, ni lazima members wale wale wareje na sio kuongeza mtu mwingine. Kwa sasa amesema wanajaribu kuurudisha urafiki tena ili waweze kufanya tena kazi vizuri.
Post a Comment
Powered by Blogger.