Cash Madame Ya Vanessa Mdee Yapeta Kwenye Chati Za Trace Naija


Vanessa Mdee anaiwakilisha Tanzania to the fullest. Wimbo wake Cash Madame unaendelea kufanya vizuri kwenye chati za muziki barani Afrika.

Wiki hii video ya wimbo huo iliyotayarishwa na Justin Campos, imekamata nafasi ya 16 kwenye chati za Urban Hit 30 za Trace Naija. Cash Madame ni wimbo utakaopatikana kwenye album yake inayosubiriwa kwa hamu, Money Mondays ambayo itaingia sokoni mwanzoni mwa mwaka 2017.


Huu umekuwa mwaka mzuri kwa Vanessa si kimuziki tu. Hivi karibuni alitajwa kuongezwa kama muigizaji wa tamthilia ya MTV Shuga na tayari yupo Afrika kushoot series hiyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.