Black Rhyno Ajipanga Kuachia Album Mwakani

 
Orodha ya wasanii watakaotoa album mwakani inazidi kuongezeka siku baada ya siku. Rapper Black Rhyno ambaye amerudi kwenye game kwa ngoma yake ya Kama Movie aliyomshirikisha Jux, ameweka wazi plan zake za kutoa pia album yake mapema mwaka 2017.

Rhyno amesema kuwa kwa sasa anatumia muda mwingi kuandaa ngoma nyingi ili kukamilisha album hiyo. Kuhusu style atakayotumia kuuza album hiyo, Rhyno amesema anafikiria kuuza online.

“Nataka ni-concetrate kwenye mauzo ya online, nataka nikae chini na kampuni mbalimbali za online music ambao wanaona tunaweza tukafanya biashara nzuri, tukakubaliana na nikaona wanaweza wakanipa faida,basi naweza nika sign nao na nikawaambia kuanzia sasa album yangu mpya itapatikana kwenye mtandao gani, amesema Black Rhyno.

 Pia amedai kuwa kuuza CD mkononi kuna Hustle zake kidogo, lakini kuuza mtandaoni ni rahisi zaidi kwani unaangalia tu album imekua downloaded mara ngapi.
Post a Comment
Powered by Blogger.