Black Chyna aanza kupewa za uso na familia ya Kardashian
Black Chyna aanza kupewa za uso na wanadada wa familia ya Kardashian kwa kutaka kulitumia jina la Kardashian.

 

Mali kubwa ambayo inawaingizia mshiko kwa sasa Khole, Kim na Kourtney ni jina lao la mwisho la Kardashian ambalo wanashare, lakini kubwa zaidi ambacho hawakitaki kutoka kwa baby mama wa kaka yao ni kwamba hawataki kumwona Black Chyna akitumia jina la ukoo wa Kardashian na hii ni baada ya Black Chyna kutaka kujiita Angela Renee Kardashian.

 

Kupitia taarifa ambazo zimenyakwa na mtandao wa Tmz zinasema kwamba Khole, Kim na Kourtney hawataki Black Chyna kutumia jina la Kardashian kutokana na kwamba wanahisi kama Chyna anataka kujipatia mafanikio kupitia jina hilo ambalo wenyewe wameliangaikia kulitengeneza kwa muda mrefu, na kubwa zaidi wanasema utumiaji wa jina hilo kwa Black Chyna utaharibu biashara zao na umaarufu.

Ishu yote hii imeanza baada ya Black Chyna kujifungua mtoto wa kwanza “Dream” kwa Rob Kardashian ambaye ni kaka wa familia hiyo inayotazamwa na watu wengi duniani kote, kilichobaki ni kusubiria hatima ya wanadada hao ambao wanapigana kuhakikisha Black Chyna hapati nafasi ya kutumia jina la Kardashian.
Post a Comment
Powered by Blogger.