Baraka The Prince Aanzisha Lebo Yake Ya Muziki ‘BANA’, Amsaini Lord Eyez


Baraka The Prince ni moja ya wasanii ambao kwa miaka miwili mfululizo amepata mafanikio ya kimuziki kwani tumeona kasaini na lebo kubwa ya muziki Afrika ya Sony Music Africa pia amekuwa kwenye menejimenti nzuri ya RockStar4000.

 Image result for baraka the prince

Kama hiyo haitoshi bado ameamua kuanzisha lebo yake ya muziki ambayo atawasimamia wasanii wenzake,Lebo yake hiyo inayoitwa ‘BANA’ yaani “Baraka and Naji” itaanza kuwasimamia wasanii wawili ambao ni Lord Eyez na Naji.

Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Baraka alisema “Nimeshafungua Recording Lebo yangu ambayo bado hatujaanza kutoa nyimbo za wasanii wetu ambao pia Lord Eyez yumo na tayari kashafanya video na Adam Juma,Pia yupo Naji kwenye lebo yangu na tayari nae kashafanya video na kwetu studio yaani tunasubiri tu mwaka ugeuke
Post a Comment
Powered by Blogger.