At adai muziki unachangamoto nyingi kuliko ndoa

 


Msanii wa bongo flava AT anasema muziki unachangamoto nyingi zaidi kuliko za kwenye ndoa au mahusiano ya mapenzi. Anasema changamoto hizo zipo hasa kwenye usambazaji wa muziki pamoja na promo, AT kazungumzia swala la mashabiki pia.

AT amesema hata mashabiki wapo wa aina mbili yaani mashabiki wa kudumu na mashabiki wa kupita njia, ambao yeye anawaita wakurupukaji.
AT

AT amesema wasanii wanatabia tofauti tofauti kuna wale wanaojiheshimu na kuheshimu mashabiki lakini pia wapo wenye dharau, kitu ambacho kinaweza kikawa chanzo cha msanii kuporomoka kisanaa.

AT amesema kuna baadhi ya wasanii wanaobebwa kwa promo za kununua ingawa hajasema ni kwa namna gani wasanii wanaweza kununua promo.

Aidha AT amesema swala la wasanii kununua promo au kubebwa na media ni aibu kwa taifa na sio kwa msanii mmoja mmoja. Kupitia ukurasa wake wa instagram AT kaandika haya

Changamoto za #Muziki ni nyingi kuliko za kwenye #Ndoa au mahusiano ya mapenzi kwani hata #mashabiki wapo aina #2 kuna #wakudumu na wapita #njia (wakurupukaji) nao #watangazaji wapo #wazalendo na #Hizbu hata wasanii wapo Wenye #dharau na #viburi hata kwa shabiki zao pia wapo wenye #upendo huru kwa yoyote pia wapo wanaobebwa na #promo za #kununua pia wapo wanaopewa support japo asilimia #40 ila mwisho wa siku km ni #Aibu zetu sote Km #Taifa la #Kitanzania Nchi Inazidi kupoteza sifa kwa Mambo madogo madogo leo Hizi zama za #Punda afe mzigo wa #bwana ufike mm nimalize kusema ( #AIBU #YANGU #NDIO #YENU #KM #MTAFIKIRIA) niwatakie jumatatu njema #2017 #kaziyao
Post a Comment
Powered by Blogger.