AlKiba atwaa tuzo mbili ASFAs 2016 Jijini KampalaSiku ya jana 09 Dec 2016 ilikua ni siku poa kwa star wa hit single ya “Aje” Alikiba kwenye ugawaji wa tuzo za AbryanzS tyle & FashionAwards (ASFAs 2016) zilizotolewa Kampala Serena Hotel.Ali Kiba

Good news ni kwamba, Alikiba kafanikiwa kuondoka na tuzo mbili ikiwemo ya Most Stylish Artiste East Africa na Most Fashionable Music Video, ambapo most fashionable music video ni video ya aje.

Huu umekua mwendelezo mzuri kwa msanii Alikiba kuufanya muziki wake kupenya nje ya mipaka ya bongo.

Hizi ni baadhi ya comment za mashabiki zake ambao waliweza kuhudhuria  kwenye ugawaji wa tuzo hizo

Kareem Nditu: kwa ujumla mchakato wa upigaji kura ulikua wazi sana na mwepesi,kuhusu kupata tuzo mbili kwa msanii kama Alikiba binafsi naona anastahili kwasababu anamashabiki wa kutosha”

Maria Funga:“Alikiba anastahili asilimia mia kwasababu kiba ni kipenzi cha watu”alimalizia shabiki huyo.

Idris sultan mchekeshaji kutoka Tanzania ndie alikua host wa tuzo hizo za ASFSs2016

Mbali na hilo kupitia EATV Awards 2016 zitakazo tolewa siku ya leo Mlimani City, Ali Kiba katajwa kuwa ni kati ya wasanii watakao toa burudani usiku huu.
Post a Comment
Powered by Blogger.