AliKiba: Sishindani na mtu kwenye muziki


Nyota wa muziki katika bongo fleva aliyetwaa tuzo 3 ikiwemo ya mwanamuziki bora wa kiume katika tuzo za EATV, Alikiba amesema hashindani na mtu yoyote kwenye muziki, bali anafanya muziki mzuri kulingana na hisia zake.

 

Kiba ametoa kauli hiyo baada ya kutwaa tuzo tatu katika tuzo za EATV na kusisitiza kuwa muziki siyo ushindani, na kwamba kinachombeba yeye ni kuwa na mashabiki wengi wanaopenda muziki wake.

Akizungumzia washindani wake katika tuzo hizo, amesema wote wanafanya kazi nzuri lakini hawana mashabiki kama yeye.

Kuhusu kuupiku wimbo wa moyo Mashine wa Ben Pol, Alikiba amesema ni wimbo mzuri huku akigoma kusema kinachofanya wimbo wake wa Aje uupiku wimbo huo wa Ben Pol.

Mbali na tuzo hiyo, kiba alishinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka na Video bora ya mwaka.
msikilize hapa Alikiba....

Post a Comment
Powered by Blogger.