Zaha aomba kuichezea timu ya Taifa ya Ivory coast badala ya Uingereza.Mcheza wa klabu ya Crystal Palace, Wilfred Zaha hatimaye amechagua kuichezea timu ya Taifa ya Ivory Coast na kuachana timu ya Taifa ya England.

Mchezaji huyo ambaye ana miaka,24, alisha wahi kucheza katika kikosi cha chini ya miaka 21 cha England na baadaye akaitwa katika kikosi cha wakubwa ambapo alicheza kwenye mechi dhidi ya Sweden Novemba 2012, na Scotland, August 2013.Hata hivyo hizo mechi zote hazikuwa za ushindani ,hivyo imekuwa si pingamizi kwa Zaha ambaye ni mzaliwa wa Abidjan,kuweza kujiunga na timu ya taifa ya Ivory Coast.

Taarifa ya Zaha kuwachagua tembo hao imethibitishwa na shirikisho la soka la Ivory Coast jana jumapili na hivyo kuweka matarajio ya kumuona akiwa na kikosi hicho kwenye michuano ya AFCON 2017, Gabon.

Zaha ambaye amezaliwa mjini Abidjan, Ivory Coast , akiwa na umri wa miaka minne walihama pamoja na familia yake kwenda mjini London na alipofikisha umri wa miaka 12 alijiunga na Academy ya Crystal Palace.
Post a Comment
Powered by Blogger.