Watu milioni 25 Tanzania wameambukizwa kifua kikuu.
Takwimu zinaonesha ya kuwa, takribani asilimia kati ya 30 na 50 ya watanzania wote tayari wameambukizwa Kifua kikuu, yaani watu wapatao million 25 hali inayotishia ukuaji wa uchumi wa taifa na shughuli za maendeleo. Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Bungeni Mjini Dodoma wakati akitoa hotuba yake kuhusu semina waliyoitoa ya kudhibiti wa ugonjwa wa kifua kikuu nchini Tanzania.

Waziri huyo ametanabaisha kuwa nchini Tanzania takriban watu 160,000 huugua kila mwaka na ni wagonjwa 62,180 sawa na 39% tu wanagunduliwa na kuwekwa katika matibabu ambapo kati yao asilimia 90 hupona kabisa.

Mhe. Mwalimu amesema kuwa makundi ya wazee, watoto, watu wanaoishi na maambukizo ya VVU, watu wenye magonjwa hatari ya kudumu kama vile kisukari na kansa, watu walio migodini, wanafunzi katika shule za bweni, wafungwa magerezani, kambi za wakimbizi, wapo katika hatari kubwa zaidi ya kuugua ugonjwa wa kifua kikuu.Katika semina hiyo iliyotolewa kwa Wabunge wa Bunge la Tanzania hapo jana wabunge hao walisaini maazimio yenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu" TB Caucus ",mtandao ulioanzishwa jijini Barcelona,Hispania Oktoba 2014 na kuitwa Mtandao wa Wabunge duniani "The Global TB Caucus.
Post a Comment
Powered by Blogger.