Ujumbe wa Van Persie kwa mashabiki wake baada ya jeraha lake baya la jicho.Robin van Persie amewaondoa hofu na wasiwasi mshabiki wake baada ya kupata jeraha baya la jicho katika mchezo wa Jumapili ya wikiendi iliyopita.
Mshambulizi huyo wa zamani wa Arsenal na Manchester United alipata ajali kwenye jicho lake katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo kati ya Fenerbahce na Akhisar Belediyespor, hali iliyomlazimu kukikmbizwa hospitali kutokana na kutokwa damu nyingi sana.

Mapema kabla ya jeraha hilo alikuwa tayari amefunga bao, lakini tukio hilo lilimfanya kutoendelea na mchezo.

Post a Comment
Powered by Blogger.