Traore ahoji kupelekwa Ajax kwa mkopo.Mshambuliaji kinda wa Chelsea, Bertrand Traore, amehoji uamuzi wa klabu yake kumpeleka kukipiga kwa mkopo katika klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi.

Kwa mujibu wa gazeti la Evening Standard, Traore, ambaye msimu uliopita alifunga mabao manne katika mechi 16 alizocheza alikuwa anauhakikika msimu huu angweza kuwamo kwenye kikosi cha kwanza cha The Blues, baada ya kucheza mechi tano za majaribio kwa ajili ya msimu huu chini ya kocha wake mpya, Antonio Conte.

Hata hivyo akajikuta Chelsea wakiingia makubaliano na Ajax akakipige kwa mkopo wa muda mrefu na kuifanya timu hiyo ibaki na mstraika wawili tegemeo Diego Costa na Michy Batshuayi.
Post a Comment
Powered by Blogger.