Timu ya Soka ya Simba SC yaitisha mkutano mkuu wa dharura.Uongozi wa klabu ya Simba umeitisha mkutano wa wanachama wa dharura utakaofanyika Desemba 11 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Msemaji wa Simba Haji Manara amesema, mkutano huo umeitishwa baada ya kikao cha kamati ya utendaji wa klabu hiyo iliyokaa Novemba 18 mwaka huu.

“Kamati ya utendaji imetoa baraka zake kupitia ibara ya 22 ya katiba ya Simba na mkutano huo utakuwa ni muendelezo wa mkutano wa kawaida uliofanyika Julai 31 mwaka huu” amesema Manara.
Post a Comment
Powered by Blogger.