Timu ya Muheza United yazindua Kombe la FA kwa kishindo.
Michuano ya Kombe la Shirikisho inayofahamika pia kama 'FA Cup' ikishirikisha timu 86 na mechi kuchezwa kwa mtindo wa mtoano katika raundi 9. imeanza rasmi kutimua vumbi lake jana katika dimba la Mkwakwani Jijini Tanga.


Katika mchezo wa ufunguzi Muheza United ya mkoani Tanga, imefanikiwa kusonga mbele katika raundi ya pili baada ya kuichapa Sifa Politani ya Temeke Dar es Salaam mabao 2-1.

Katika mchezo huo ambao haukuwa na ushindani sana, Sifa ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 22, kabla ya Muheza kubadilika kipindi cha pili na kupata mabao mawili dakika ya 70 na 80.

Kwa matokeo hayo Sifa Politan inafungasha vilago, ambapo nahodha wake mkongwe Salum Kinje ambaye amewahi kukipiga timu ya Simba, na Taifa Stars, amekiri kuzidiwa mbinu na Muheza United, huku akisema Muheza wametumia nguvu zaidi kutafuta mabao na kuwazidi mabeki wa timu yake, na kwamba watajipanga upya licha ya kuwa hilo halikuwa lengo lao.
Post a Comment
Powered by Blogger.