TIC Yazindua Kitengo Cha Huduma Za Mahala Pamoja Ambapo Huduma zote za uwekezaji Zitapatikana sehemu moja


Idadi ya siku na utaratibu unaotumika kuomba vibali vya uwekezaji nchini Itapungua baada ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kufungua huduma ya mahala pa kutolea huduma za pamoja.


Katika huduma hiyo vibali kutoka taasisi zote zinazohusika na uwekezaji nchini zitapatikana katika sehemu moja.


Waziri ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ndiye aliyefungua kituo hicho jijini Dar es Salaam jana ambapo katika maelezo yake alizitaka taasisi za umma kufanya kazi kwa ushirikiano ili kupunguza urasimu usio wa lazima na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara.


Awali akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw. Clifford Tandari alisema wao kama kioo cha wafanyabiashara wanaokuja kuwekeza nchini wamejipanga kuhakikisha kuwa huduma wanazotoa zinachochea ukuaji wa uchumi kama yalivyo matarajio ya serikali.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Bw. Godfrey Simbeye aliipongeza hatua hiyo ya serikali na kwamba inaonesha matumaini ya kufikia uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni 25 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Waziri wa Viwanda na Biashara ,Charles Mwijage, akizungumza na baadhi ya watoa huduma katika Kitengo hicho mara baada ya uzinduzi wake.
Post a Comment
Powered by Blogger.