Taarifa za majeraha ya Garreth Bale kuelekea mechi ya El Classico.


Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale ambaye yupo shakani kuukosa mchezo wa mwishoni mwa juma lijalo dhidi ya FC Barcelona.

Bale aliumia kifundo cha mguu katika mchezo wa mzunguuko wa tano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Sporting Lisbon, uliochezwa jumanne mjini Lisbon.

Tovuti ya klabu ya Real Madrid imetoa taarifa ambazo zimeeleza kuwa, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 huenda akapata ahuweni na kuwahi mazoezi ya kikosi cha Real Madrid kuelekea katika mchezo wa El Classico.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa “Bale atakua chini ya uangalizi wa kitatibibu na huenda kaanza mazoezi mepesi, kulingana na matarajio ya kupata ahuweni ya jerahe lake la kufundo cha mguu, ”

“Kuna uwezekano mkubwa wa kuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kuelekea mjini Barcelona Disemba 03.” Ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeleta mashaka miongoni mwa mashabiki ambao wanahisi huenda kuna ajenda ya makusudi ya kumuharakisha Bale ili acheze mchezo dhidi ya FC Barcelona, jambo ambalo wanahisi litawagharimu kwa kiasi kikubwa na kuhatarisha afya ya mshambuliaji huyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.