Stand United, Prisons zamgombea Busungu.


Timu za Stand United na Tanzania Prisons zinawania kumtwaa kwa mkopo mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu, katika kipindi cha dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Busungu alisajiliwa na Yanga katika  msimu uliopita akitokea JKT Mgambo, lakini anaonekana kusugua benchi kutokana na ushindani wa namba kutoka kwa washambuliaji wenzake, Obrey Chirwa, Amisi Tambwe na Donald Ngoma.
Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana zilieleza kuwa klabu hizo zimepeleka barua  kwa uongozi wa Yanga ya kumwona mshambuliaji huyo.
Kocha wa Stand United, Athuman Bilali,  alikiri kumhitaji Busungu ili aweze kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
“Ni mchezaji mzuri, nimependekeza katika ripoti yangu namhitaji katika kikosi changu,” alisema Bilali.
Kwa upande wa  Busungu alisema ana mkataba na Yanga utakaomalizika msimu huu, lakini haumzuii kuondoka na  kama timu inayomhitaji itamalizana na mabosi wake.
Post a Comment
Powered by Blogger.