Shirikisho la soka TFF kuongeza nguvu mafunzo ya soka la wanawake


Shirikisho la Soka nchini TFF limesema mara baada ya kumalizika kwa kozi ya awali ya mafunzo ya soka kwa wanawake sasa wanalenga kuwa na kozi nyingine mbalimbali kwa upande wa soka la wanawake ili kuhakikisha soka hilo linakua zaidi nchini.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa kufunga kozi ya mafunzo ya soka kwa wanawake, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Celestine amesema, kozi hizo zitalenga kuelimisha jamii kuhusu soka la wanawake pamoja na kulitangaza nchi nzima hususani vijijini.

Mwesigwa amesema kozi zitakazofuata zitahusisha masuala ya lishe pamoja na tiba kwa upande wa soka la wanawake ili kuhakikisha wanakuwa na madaktari pamoja na watu watakaohusika na lishe kwa wachezaji hapa nchini.Celestine Mwesigwa (Kulia) - Katibu Mkuu TFF

Mwesigwa amesema, pia ubalozi wa nchini Sweden umeahidi kushirikiana na TFF ili kuhakikisha rasilimali zinapelekwa katika soka la wanawake ili kulikuza na kulisambaza zaidi hapa nchini.
Post a Comment
Powered by Blogger.