Samuel Umtiti kukosa michezo mitano ya klabu yake ya Barcelona..Klabu ya soka ya Barcelona imepata pigo jingine kwenye eneo la ulinzi baada ya beki wake tegemeo kwa sasa Mfaransa Samuel Umtiti kuumia akiwa kwenye mazoezi na kikosi cha Timu ya Taifa ya Ufaransa.


Barcelona ambayo inaendelea kumkosa beki wa kati Gerrad Pique na beki wa kushoto Jordi Alba walioumia kwenye mchezo wa kwanza wa UEFA dhidi ya Manchester City uliopigwa Camp Nou mwezi Oktoba itakuwa kwenye wakati mgumu ambapo Umtiti atakaa nje kwa muda wa wiki tatu.
Taarifa ya klabu imesema Umtiti ameumia goti la kushoto akiwa kwenye mazoezi ambapo timu yake inajiandaa kuikabili Sweden usiku wa leo. Kuumia kwa Umtiti ni mwendelezo wa matatizo ya goti lake la kushoto ambapo mwezi Septemba aliumia na kukosa mchezo dhidi ya Atletico Madrid.


Umtiti atakosa mchezo wa kirafiki kati ya Ufaransa na Ivory Cost Novemba 15 pamoja na ile ya Ligi Kuu ya Hispania pamoja na UEFA dhidi ya Malaga, Celtic, Real Sociedad na Hercules. Tayari nafasi ya Umtiti imezibwa na beki wa Valencia Eliaquim Mangala.
Post a Comment
Powered by Blogger.