Sababu za shirikisho la soka TFF kumsimamisha mchezaji kujihusisha na soka.Mara baada ya timu ya Panone FC kupeleka malalamiko juu ya ushiriki wa mchezaji Christopher Mahanga katika Ligi ya TFF ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20, Shirikisho la Soka nchini TFF limesimamisha ushiriki wa mchezaji huyo katika mashindano.

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema, timu ya mpira wa miguu ya Panone ya Moshi ilipeleka malalamiko yake mara baada ya kushangazwa na mchezaji huyo kuibukia timu ya Kagera ambayo ilikuwa ikipambana na Yanga ilihali akidaiwa kuwa na usajili katika timu hiyo kwa msimu wa pili mfululizo.

Alfred amesema, idara ya Mashindano ya TFF imebaini kuwa mchezaji huyo alikuwa na usajili kwa timu zote mbili kwa usajili wa majina tofauti ilihali picha ikionekana kuwa mmoja ambapo Panone FC alisajiliwa kwa jina la Christopher Mshanga kuanzia msimu wa 2015/2016 na pia msimu wa 2016/2017.

Alfred amesema, taarifa za awali ambazo TFF ilizifanyia kazi zinasema kwamba baada ya kusajili Panone FC ya Moshi, akachezea timu mbili na kuaga kuwa amekwenda kutibiwa majeraha, lakini wakati anasubiriwa, amekuja kuonekana kwenye mchezo ambao Kagera ilikuwa ikicheza na Young Africans katika mashindano ya ligi ya vijana wa U20 ya TFF.

Alfred amesema, mchezaji huyo amesimamishwa mpaka Novemba 28 mwaka huu huku uchunguzi ukiendelea na iwapo katika uchunguzi huo itagundulika ni kweli mchezaji huyo alifanya udanganyifu atakuwa katika hatari ya kufungiwa kucheza soka kwa muda wa mwaka mmoja huku Kagera Sugar ikiondolewa pointi tatu pamoja na viongozi waliohusika kumsajili kuchukuliwa hatua.
Post a Comment
Powered by Blogger.