Nchi nne Afrika zathibitisha kushiriki ngumi Dar Es Salaam.Mashindano ya Bingwa wa Mabingwa ya mchezo wa Ngumi yanatarajiwa kuanza Desemba tisa mpaka 15 mwaka huu jijini Dar es salaam kwa kushirikisha mabondia mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Rais wa Shirikisho la Ngumi nchini BFT Muta Lwakatare amesema, mashindano hayo yanatarajia kushirikisha nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika na mpaka muda huu ni nchi nne pekee zilizohakiki ushiriki wa mashindano hayo ambazo ni Cameroon, Kenya, Uganda na Rwanda.

Muta amewataka mabondia watanzania watakaoshiriki katika mashindano hayo kufanya mazoezi kwa bidii ili kuweza kufanya vizuri katika mashindano hayo yenye lengo la kupata mabondia watanzania watano wenye uwezo wa kupambana ambao wataingia kambini nchini Cuba kwa ajili ya maandalizi ya mashindano yajayo ya Olimpiki yatakayofanyika mwaka 2020 Tokyo nchini Japan.
Post a Comment
Powered by Blogger.