Mipango anyoipanga Gianni Infantino kuhusu kombe la dunia na vilabu.

Gianni Infantino ana mpango michuano ya Kombe la Dunia kwa upande wa klabu, iwe na timu 32, Infantino anataka timu ziongezeke kutoka saba hadi 32 ili kuongeza utamu na mpango wake anataka uanze mwaka 2019.

Infantino ameliambia gazeti la michezo la Gazzetta dello Sport na lile la El Mundo Deportivo kwamba anaamini hilo linawezekana.

Michuano ya Kombe la Dunia la klabu mwaka 2015 iliyofanyika nchini Japan kama ilivyo ada, iliingiza faida kupitia matangazo kiasi cha dola million 20 ambacho kilionekana ni kiasi kidogo kwa kuwa michuano ya mwaka 2014 iliyofanyika nchini Morocco iliingiza hadi dola million 40.
Post a Comment
Powered by Blogger.